Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulimboka amuonya Mbelgiji wa Simba

89767 Ulimboka+pic Ulimboka amuonya Mbelgiji wa Simba

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kocha wa AFC Arusha Ulimboka Mwakingwe amesema mchezo wao dhidi ya Simba si kipimo kwa Sven Vanderbroeck.

Ulimboka alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumzia kipigo cha mabao 6-0 ilichopata AFC Arusha katika mchezo wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, juzi.

Sven alisema amefurahishwa na matokeo hayo, lakini Ulimboka alisema mechi hiyo haikuwa kipimo kwa kocha huyo kwa kuwa wachezaji wake hawakufanya mazoezi muda mrefu.

Winga huyo wa zamani wa Simba, alisema alitarajia Simba ingeshinda mabao 10 katika mchezo huo kutokana na kikosi chake kutokuwa kambini wiki tatu.

“Simba wasijisifu kutufunga mabao 6-0 kama kipimo cha ubora wao, timu haikuwa na mazoezi zaidi ya wiki tatu. Binafsi sikukaa katika benchi kwa kuhofia aibu, lakini napongeza wachezaji wamepunguza idadi ya mabao,”alisema Ulimboka.

Alisema timu hiyo ilikwenda Dar es Salaam kwa mafungu matatu wakitokea Arusha, Morogoro na jijini humo na wachezaji hawakuwa fiti kwa mchezo wa mashindano.

Kocha huyo alisema AFC Arusha inakabiliwa na ukata muda mrefu na mara kwa mara amekuwa akitoa fedha za mfukoni kuihudumia.

Chanzo: mwananchi.co.tz