Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiona Kagere kaziba jicho Simba kaua

14336 Pic+jicho TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtindo wa ushangiliaji wa kuziba jicho mmoja wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere umeanza kuteka hisia za mashabiki wake.

Kagere alianza kufanya hivyo katika mashindano ya Kombe la Kagame ambapo Simba ilimaliza mshindi wa pili, huku Azam FC ikitetea ubingwa wa taji hilo, alikuwa akifunga bao anajiziba jicho moja, wakati mwingine anatembea kama ameshika mkongojo.

Baada ya jana Jumatatu Kagere kuifungia timu yake mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City, mashabiki Simba walianza kuigiza mtindo wake ya kuziba jicho moja, huku wakiungana naye katika furaha yake.

Katika pita pita mtaani Mwanaspoti limebaini namna mtindo huo ilivyopata umarufu kwani katika vijiwe utawasikia ukimuona Kagere kaziba jicho moja ujue Simba imeralua mtu.

Mwanaspoti imewahi kumuuliza Kagere kuhusiana na aina hiyo ya ushangiliaji, aliifafanua kuwa akiwa na furaha na hasa akatimiza malengo yake uwanjani basi furaha yake anaiwasilisha kwa staili hiyo.

"Napenda kufanya kazi nzuri na zenye viwango vya juu, mtindo zangu zote ninazoshangilia ndani yake zinakuwa zimebeba furaha, sipendi kufanya kazi kwa ulegevu," alisema Kagere.

Chanzo: mwananchi.co.tz