Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukata waiweka sokoni Kiluvya FC

Tue, 20 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kikosi cha wachezaji 14, Kocha Mkuu na Katibu wa Kiluvya United kimekwama Ruvuma baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Mlale FC mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na ukata unaowakumba hivi sasa.

Katibu wa Kiluvya, Omari Masawila alisema ligi imekuwa na gharama kubwa kuliko faida wanayoipata na vyema TFF wakaliangalia mapema kwani kuna timu nyingi zitaishia njiani.

"Baada ya kutoka Mbeya tulipokwenda kucheza na Mbeya Kwanza tukaona ni vyema tubaki huku kwaajili ya mchezo dhidi ya Mlale FC, hata hivyo tumejikuta tukikwama kwa sababu ya bajeti yetu kuwa finyu,"

"Tumekaa nje ya Pwani kwa zaidi ya siku 10 sasa na hatujui itakuaje ndio maana tunaomba wadau watusaidi kuirudisha timu nyumbani kwani mambo yametuzidi hovyo hapa tulipo," alisema Masawila.

Aliongeza kutokana na hali ya uchumi kuzidi kuwa mbaya, wanaiweka timu hiyo sokoni kuanzia sasa na mtu yoyote anakaribishwa kuinunua kwani wao imewashinda kuiendesha.

"Tumeona bora kuiuza kuliko kuiacha hivi ilivyo halafu ikashushwa, timu haina tatizo lolote zaidi ya ukata ndio maana tumeamua kuweka wazi ili wadau watusaidie huu mzigo."

Timu hiyo ilianzishwa mwaka 2012 na inashiriki FDL msimu wa tano sasa huku ikiwa na pointi tano baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoa sare mbili katika michezo saba waliocheza msimu huu.

Masawila aliongeza kuwa kama hawatapata mteja kuna hatari kubwa timu hiyo kushindwa kuendelea na ligi na wapo tayari kwa lolote litakalowatokea na hapo ndio historia ya Kiluvya FC inaweza ikafika ukingoni.



Chanzo: mwananchi.co.tz