Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Gerson Msigwa kwa wasemaji wa vilabu

Msigwa Ujumbe wa Gerson Msigwa kwa wasemaji wa vilabu

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: eatv.tv

Aliyewahi kuwa msemaji wa timu ya Maji Maji ya mkoani Ruvuma na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ambaye hivi sasa ni msemaji wa serikali, Gerson Msigwa amewasihi wasemaji na wakuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa vilabu vyetu nchini kutenda kazi kwa weledi ili kuinua soka nchini

Submitted by George David on Alhamisi , 29th Jul , 2021 Mdau mkubwa wa michezo ambaye hivi sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Msigwa ameyasema hayo usiku wa jana wakati alipokuwa anaunguruma kwenye moja ya kipindi bora cha michezo nchini cha 'KIPENGA' cha East Africa redio kwenye masafa ya 88.1 jijini Dar es Salaam.

Msigwa amesema kitengo hicho ni muhimu sana kwa timu zetu kwasababu wataalamu wa mawasiliano ndiyo wanaopaswa kuandaa mipango mikakati ya mawasiliano ili kuvutia wawekezaji na watu wa maendeleo kwenye vilabu vyetu.

Msemaji huyo wa serikali kwa sasa ambaye ni shabiki wakutupwa wa mchezo wa soka amewatumia ujumbe wasemaji na wadau wa michezo nchini kwa kuanza kugusia makujumu na kazi za Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano na wasemaji wa vilabu.

“Yeye kazi yake ni kufanya mawasiliano kati ya klabu, wapenzi wa klabu, wanachama, kuunganisha mipango, kuitangaza timu katika sura inayovutia”

“Lakini muhimu zaidi kitaalamu, yeye sasa ndiye anayetengeneza mipango mikakati ya kimawasiliano kwa timu. Mfano timu inataka kutafuta fedha, inataka udhamini, yeye anatengeneza mpango mkakati wa kimawasiliano utakaoisaidia timu kuwavutia wawekezaji na watu wanaotaka kuchangia maendeleao yake”

“Pia ndiye atakayetengenza mpango mkakati wa kufanya mashabiki waishangilie timu waungane na wachezaji wakati wote wa ushindi na kushindwa. Usipofanya hivyo wewe timu itashangiliwa ikishindwa itazomewa sana ikishindwa.”

“Kwahiyo kitengo hiki ni muhimu sana kwa timu kwasababu timu ni chombo ambacho kinahitaji mawasiliano ya karibu kati ya watu wanayoishabikia na wewe ambaye  unayeiongoza”

“Vinginevyo usipofanyakazi yakeo vizuri utajikuta uongozi timu yako ipo kwenye misuko suko na wanachama au mashabiki wake kwasababu hakuna mtu anayeeleza mipango mbalimbali kwasababu zake ili wanachama wawe sehemu ya ushindi na kushindwa kwa timu.”

Mwisho, Msigwa akawasihi wasemaji wa vilabu hivyo kuendelea kusimamia weledi kwenye utendaji wake.

“Waendelee kufanyakazi kwa weledi waendelee kuuza timu zao, wawe na mipango mizuri”.

Chanzo: eatv.tv