Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufalme wa Makambo wazimwa Rwanda, wachapwa 1-0

14585 Pic+yanga+rayol TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mkongo Haritier Makambo ameshindwa kuisaidia klabu yake ya Yanga ambayo imechapwa bao 1-0 na Rayon Sports ya Rwanda katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Nyamirambo.

Yanga walicheza mchezo huo kwa ajili ya kukamirisha ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kutokana na kutofanya vizuri katika michezo yao iliyopita.

Mshambuliaji huyo mpya wa Yanga anayeaminiwa zaidi na mashabiki wa klabu hiyo kwa sasa, alijikuta ufalme wake ukizimwa na Wanyarwanda hao kupitia kwa Mrundi Mrundi Caleb Bimenyimana aliyefunga bao hilo dakika ya 18.

Makambo anayevaa jezi namba 19 katika mashindano hayo na 11 kwenye ligi kuu, alitolewa dakika ya 67 na nafasi yake ilichukuliwa na Yusuf Mhilu.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na mvua za hapa na pale hali iliyosababisha uwanja kujaa maji, Bimenyimana aliyezaliwa Novemba 21, 1997 aling'ara.

Katika mchezo huo, kwa mara ya kwanza, kocha Mkongo Mwinyi Zahera alionekana akiiongoza Yanga akiwa amekaa kwenye benchi la ufundi. Zahera alishindwa kukaa kwa sababu hakuwa na kibali cha kazi.

 

RAYON NA USM ALGER ZASONGA

Kutokana na matokeo hayo, timu za Rayon na USM Alger ndiyo zinasonga mbele hatua ya robo fainali. USM Alger wameifunga Gor Mahia mabao 2-1.

Chanzo: mwananchi.co.tz