Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Yanga mambo ni moto, mambo ni fire

Suma1 Pic Data Suma Mwaitenda

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgombea makamu mwenyekiti wa Yanga, Suma Mwaitenda amesema anajiamini na ana sababu zilizomfanya ajitokeze kuwania nafasi hiyo, jambo la msingi ni wajumbe kumpigia kura.

Amesema ana mambo mengi anayotamani kuifanyia Yanga endapo akipata nafasi ya kuchaguliwa na amevitaja vipaumbele vyake.

Jambo la kwanza alitaja ni kumsaidia Rais kutekeleza majukumu ya mipango ya maendeleo ya klabu, kudumisha mshikamano na umoja wa wanachama na wawekezaji,kuongeza ushawishi na kuongeza mashabiki wapya katika taswira ya soka lenye ushindani,  kuboresha namna Bora ya mawasiliano kati ya mashabiki,wanachama, wawekezaji na viongozi wa klabu.

Mengine ni kusimamia maslahi ya wananchi na wanachama katika uwekezaji wa klabu,kumpigania maendeleo na mafanikio ya timu ya klabu (Yanga Senior, Yanga Junior na Yanga Princess) na kuongeza vyanzo vya mapato katika timu yetu.

Kuongoza sera maaluuma kwa ajili ya kukuza vipaji vipya katika taswira ya soka lenye ushindani,  kuongeza vyanzo vipya vya mapato katika klabu.

"Kupitia talaamu yangu endapo nikifanikiwa kuchaguliwa natamani kutoa mchango wa kuisaidia Yanga katika nyanja mbalimbali," amesema.

Mbali na hilo, amesema jambo la msingi kwake ni baada ya uchaguzi Yanga itabakia  moja na mambo mengine yatakaa pembeni na amewasisitiza wajumbe waangalie wagombea wa kuleta mafanikio ndani ya klabu.

"Uchaguzi ukimalizika tutabakia kuijenga Yanga moja iwe mimi ama wagombea wengine, hizo kampeni zikipita kitakachobakia ni kufanya kazi kwa bidii,"amesema.

Ameulizwa je, kitendo cha mgombea Urais injia Said Hersi kuongozana na Arafat Haji anayegombea umakamu kama kinampa changamoto? Amejibu "Najiamini kupitia hoja zangu ninazonadi, hivyo wajumbe watachagua anayewafaa."

Ameongeza "Kitu wanachotakiwa kufahamu watu ni kwamba bado Hersi hajawa mwenyekiti hadi zitakapopigwa kura Julai 9, ila kwa sasa kila mtu anafanya kampeni."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live