Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UBISHI WA MZEE WA KALIUA: Baada ya kumtimua Kaze, anayefuata ni GSM?

Kslius Pic Data UBISHI WA MZEE WA KALIUA: Baada ya kumtimua Kaze, anayefuata ni GSM?

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

HUWEZI kujua. Yanga wa misimu hii mitatu usiiamini sana! Imekaa kikorofi korofi. Imekaa kihasira hasira! Imekaa kipresha presha.

Tayari Yanga imetimua makocha watano katika kipindi cha miezi 16 ya hivi karibuni, lakini sioni sababu yoyote ya msingi ya timua timua hiyo, Yanga wamekuwa wakali. Yanga wamekuwa wakorofi, kimahesabu, Yanga wanatimua kocha kila baada ya miezi mitatu.

Kwa timu ambayo zaidi ya asilimia 70 ya wachezaji wake ni wageni kwenye timu na ligi, ni vigumu sana kufanikiwa. Yanga walianza kwa kumtimua Kocha Mwinyi Zahera baada ya sare moja na kufungwa moja.

Kulikuwa na sababu kweli hapa ya kumtimua kocha? Usinipe jibu. Alifuata Charles Boniface Mkwassa na matokeo mazuri tu lakini aliondolewa. Shughuli ikaenda kwa Luc Eymael ambaye naye akatupiwa virago, Hii ndiyo timu ya Wananchi.

Imekaa kikorofi korofi sana siku hizi. Imekaa kihasira hasira sana siku hizi. Alikuja Zlatko Krmpotic, moja ya makocha wazuri tu. Aliiongoza kwenye mechi tano za ligi, alipata ushindi mara nne na kutoka sare mara moja lakini akatimuliwa. Kufukuza makocha haijawahi kuwa msaada hata kidogo kwa Wananchi, ni hatua mbili kurudi nyuma.

Kulikuwa na sababu kubwa mbili zilizochangia kwa kiasi kikubwa Yanga kuyumba kwa misimu mitatu ya hivi karibu, kwanza ni hali ngumu ya kiuchumi na pili, ni kukosa wachezaji bora wa kuweza kushindana uwanjani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz