Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo ya Samatta Ulaya yamuongezea kasi Kelvin John

56151 Pic+samatta

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta wa timu ya Taifa Tanzania na klabu ya KRC Genk, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo (Eboy Shoe Award 2019) ya mchezaji bora wa mwa Kiafrika anayecheza  nchini Ubeligiji.

Baada ya kuchukua tuzo hiyo, imemfanya nyota chipukizi wa Serengeti Boys, Kelvin John ‘Mbappe’ akubali mziki wa Samatta ambao ameuonyesha msimu huu katika Ligi Kuu ya Ubeligiji.

Mbappe baada ya kupata taarifa za Samatta kupata tuzo hiyo, alisema kwa namna ambavyo  amepambana (Samatta) ana kila sababu ya kupewa tuzo bila kikwazo chochote.

“ Hongera sana kwake na kiukweli alistahili kuchukua hii tuzo kwa kitu ambacho amekionyesha msimu huu, amepambana na kila mtu ameona nini ambacho amekifanya,” alisema.

Mbappe aliongeza kupitia kwa Samatta amejifunza kuongeza nidhamu katika kazi pamoja na kujituma muda wote ili kufika katika lengo ambalo amejiwekea.



Chanzo: mwananchi.co.tz