Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

''Tutaenda kombe la dunia'' - Pawasa

Pawasa.jpeg ''Tutaenda kombe la dunia'' - Pawasa

Tue, 25 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya taifa ya soka la Ufukweni ya Tanzania inashuka dimbani leo Mei 24, 2021, kukabiliana na Uganda wakiwa na matumai kibao kushinda mechi hii ya BS AFCON nchini Senegal.

Akizungumza na Kipenga ya East Africa Radio kinachoruka kila siku ya jumatatu hadi ijumaa kocha wa timu hiyo Boniface Pawasa alisema '' hatuwaogopi Uganda ni wenzetu wa ukanda moja na kiufundi wapo chini ya kiwango chetu ukilinganisha ''

''Tunaanza safari yenye matumaini leo hii jioni, tunaomba Watanzania huko nyumbani kwa imani tofauti za dini zenu mtuombee, kwa upande wetu huku kila kitu kinakwenda vizuri'aliongeza kocha Pawasa

Michuano hiyo ya soka la ufukweni inayofanyika nchini Senegal ilianza jumapili hii tarehe 23/5/2021 kwa kushuhudia wenyeji wakipata ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Uganda,huku kundi B, Msumbiji waliwafunga Misri 7-5 na Morocco alimfunga Shelisheli 5-1.

Mashindano haya ya soka la ufukweni kwa Afrika 'BSAFCON' hutumika kupata timu zitakazo wakilisha katika mashindano ya dunia ambayo kwa mwaka huu yatafanyika katika mji wa Moscow nchini Urusi kuanzia kuanzia tarehe 19-29 mwezi wa 8 .

 

 

 

 

Chanzo: eatv.tv