Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshishimbi kutua AS Vita

TSHISHIMBI Tshishimbi kutua AS Vita

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: mtanzania.co.tz

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi,ameweka wazi kuwa kama mambo yatakwenda vizuri atajiunga na Klabu ya AS Vita ya nchini kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Tshishimbi aliondoka jijini Dar es Salaam juzi kurejea DRC,akiwa na mshambuliaji David Molinga.

Tshishimbi na Molinga walipewa mkono wa kwaheri na Yanga,baada ya mikataba yao kumalizika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipofika tamati.

Tshishimbi ambaye ni kiungo alishindwa kuafikiana kwenye maslahi,wakati Molinga alitemwa kutokana na kutokidhi matarajio dimbani.

Akizungumza na TANZANIA kabla ya kutimkia DRC, Tshishimbi alisema kuwa wakala wake ameanza mazungumzo na AS Vita, ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

“Wakala wangu ameniambia kuna timu mbili zinanihitaji kule nyumbani mojawapo ni AS Vita, sijaona kama ni tatizo nitaenda kufanya kazi huko kama mazungumzo yatakwenda vizuri.

“Nawashukuru Watanzania hususani mashabiki wangu wa Yanga walioonyesha mapenzi kwangu naahaidi kuwaheshimu na kuwapenda siku zote, kwa sababu nina uhakika ipo siku nitarudi tena Tanzania kufanya kazi,”alisema Tshishimbi.

Chanzo: mtanzania.co.tz