Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshishimbi awainua Yanga

12131 Yanga+huko+moro+pic TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Katika mechi ya Kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Mkamba Rangers mpaka sasa dakika ya 70, Yanga wapo mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo mkabaji Papy Kabamba 'Tshishimbi' dakika ya 82 pasi kutoka kwa Deus Kaseke.

Mechi hiyo pia itatumika kwa ajili ya kumuaga, Nadir Harub 'Canavarro' ambaye anakwenda kuchukua nafasi ya maneja ambayo awali ilikuwa chini ya Hafidhi Saleh ambaye kwa sasa atakwenda kuchukua nafasi ya Uratibu.

Yanga katika mechi hii wamewapa zawadi ya mipira miwili Mkamba Rengers.

Mechi inakuwa ya pili ya kirafiki kwa Yanga baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro siku ya Jumamosi.

Baada ya mechi hii Yanga watarudu Dar es Salaam na siku ya Jumapili watacheza dhidi ya USM Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika huku wakiwa na kumbukumbu ya kuchezea kichapo cha mabao 4-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza ambayo ilichezwa nchini Algeria.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz