Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshishimbi, Kamusoko wasakwa kila kona

14465 Pic+tshioshimbi TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigali. Yanga imewasili salama tayari kwa kuwavaa wapinzani wao Rayon Sports katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Ingawa kikosi hicho kimewaacha nyota wake kadhaa kwa sababu mbalimbali, kuna wachezaji wawili wa viungo ambao wamekuwa gumzo zaidi mjini hapa.

Tangu wakiwa uwanja wa ndege, maofisa wa chama cha soka hapa Rwanda na wenyeji wao walionekana kumuulizia zaidi kiungo Papy Tshishimbi baada ya kutomuona wakiamini amefichwa ingawa hayumo katika msafara.

Mbali na Papy raia wa DR Congo mchezaji mwingine waliyekuwa wakimulizia ni kiungo Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe.

Maofisa hao walionekana kumsifu Kamusoko wakikumbuka alivyoifunga bao APR ya hapa msimu mmoja uliopita wakati Yanga ilipopata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1.

Kocha Mwinyi Zahera ameliambia gazeti hili kukosekana kwa viungo hao kunatokana na sababu mbalimbali za binafsi.

Mbali na viungo hao pia Zahera alisema Yanga itamkosa nahodha wake msaidizi Juma Abdul mchezaji anayekumbukwa hapa kutokana na bao lake la mbali alilowatungua APR.

Beki huyo wa kulia ameachwa kutokana na kuwa majeruhi wakati Haji Mwinyi amekwenda Zanzibar kumuuguza mzazi wake.

Mwinyi alisema Said Juma ‘Makapu’ hakuwa sehemu ya msafara wao kutokana na kufiwa na mama yake mzazi na amekwenda Zanzibar kushiriki mazishi.

Alisema licha ya kukosekana wachezaji hao, ana matumaini ya kupata pointi tatu kutokana na morali ya wachezaji.

Yanga imetua hapa ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Algier ya Algeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz