Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala atoa ya moyoni Simba

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amedai matokeo iliyopata katika mechi tatu, zimewapa morali ya kuongeza kwenye michezo mingine inayofuata ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza Dar es Salaam jana, beki huyo wa kushoto, alisema Simba matokeo dhidi ya Ndanda, Mbao na Yanga hayakuwa mazuri, lakini watapambana kurejea katika mstari.

Tshabalala alisema Simba ina nafasi ya kutetea ubingwa licha ya kuambulia pointi mbili katika mechi hizo dhidi ya Ndanda na Yanga ambazo timu hizo zilitoka suluhu.

Simba inayonolewa na Kocha Patrick Aussems, ilifungwa bao 1-0 na Mbao FC mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

“Tumepata uchungu baada ya kufungwa na Mbao, pia matokeo ya sare mechi mbili yametupa uchungu, lakini tumejipanga kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo,” alisema nahodha huyo msaidizi.

Beki huyo alisema Simba ina changamoto ya kuwania ubingwa kwa kuwa mashindano hayo msimu huu ni magumu na timu imejiandaa vyema kushinda katika kila mchezo.

Timu hiyo inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 11 katika mechi sita ilizocheza msimu huu.

Simba ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kutoka mikononi mwa watani wao wa jadi Yanga baada ya kusotea kwa miaka mitano tangu mwaka 2012.

Chanzo: mwananchi.co.tz