Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu za Taifa zifanye maandalizi ya Kutosha

01 1 1140x640 Timu za Taifa zifanye maandalizi ya Kutosha

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: dar24.com

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Buyungu, wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Mhe. Aloyce Kamamba amesema timu zote za taifa zifanye maandalizi ya kutosha ili kuwakilisha vema taifa katika mashindano ya kimataifa.

Mhe. Kamamba amesema hayo Septemba 2, 2022 baada ya kupokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa na Wizara hiyo kwenye kamati hiyo kuhusu utendaji wa taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

“Sisi kama kamati tumesisitiza Wizara kwamba timu zote za taifa ziwe za wanawake,wanaume ama walemavu zipate muda wa kutosha kwa ajili ya maandalizi, isiwe muda mfupi. Ipate muda wa maandalizi wa kutosha pamoja na fedha ili kile cha muhimu katika timu hiyo kama imeandaliwa vizuri kiweze kupatikan.a kwa timu kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali” amesema Mhe. Kamamba.

Timu hizo za taifa zinasimamiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ni muhimu kwa taifa katika kusimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema siri kubwa ya mafanikio ya Wizara hiyo ni ushirikiano mkubwa kati ya Viongozi wa Wizara na watumishi wote kuhakikisha malengo ya kuwatumikia watanzania katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo yanafikiwa.

Ili kuhakikisha vipaji vya Sanaa na Michezo kwa vijana vinaendelezwa, Naibu Waziri Mhe. Gekul amesema wanafunzi wanaofanya vizuri katika mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA wataendelezwa kuptia shule maalum za michezo 56 ambazo ni mahususi kwa kuendeleza vipaji vya Sanaa na Michezo.

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu amesema kuwa Wizara imetenga bilioni 2 kuhakikisha shule 56 za kulea vipaji vya wanamichezo zinakuwa na miundombinu ya michezo ambayo itasaidia kukuza na kuendeleza vipaji michezo mbalimbali nchini na kuongeza kuwa Wizara hiyo imetenga kiasi cha Bilioni 10 kuhakikisha kunakuwa na viwanja saba vyenye ubora unaotakiwa kimataifa kwa michezo mbalimbali.

Chanzo: dar24.com