Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Thomas Lemar kuchukua nafasi ya Coutinho Liverpool?

1128 Liver 615x400 TZW

Fri, 5 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Bado taarifa za mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil na Klabu ya Liverpool  Philippe Coutinho anaendelea kuzishikilia headlines za usajili Barani Ulaya ambapo sasa ni Wamiliki wa Liverpool wamepanga siku ya leo kumpatia Jurgen Klopp maamuzi yao ya mwisho kuhusu Coutinho kama ataondoka katika dirisha hili dogo la usajili.

Gazeti la The Times zimeripoti taarifa inayosema kuwa Liverpool wapo tayari kupokea dau la paundi milioni 133 za usajili wa Coutinho lakini pia Klopp ana uwezo wa kuikataa ofa hiyo.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa Barcelona wameonyeshwa kukerwa na mshahara ambao Coutinho atalipwa kama atajiunga na Barca. Mshahara ambao wamepanga kumlipa mchezaji huyo ni kiasi cha paundi milioni 10.5 kwa mwaka kwa taarifa ambazo zimetolewa na mtandao wa Hispania wa Diaro Gol.

Liverpool wameanza kumuwinda nyota wa Monaco, Thomas Lemar kwa ajili ya kuziba pengo la Coutinho endapo ataondoka na watalazimika kulipa kiasa cha paundi milioni 90 kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo.

Lemar (22) amekuwa akiwindwa na Liverpool pamoja na Arsenal kwa muda lakini sasa nyota huyo wa Ufaransa anadaiwa kuchagua kutua Anfield kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Daily Express.

VIDEO: SPORTPESA TANZANIA WAMEONGEA BAADA YAA KAMPUNI YAO KUJITOA UDHAMINI KENYA

NAHODHA WA TIMU YA SOKA YA WANAWAKE WA AUSTRIA AMETUA AMEELEZA HAYA KWA WATANZANIA

Chanzo: millardayo.com