Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tenga, Ndolanga ndani TFF

39762 Tenga+pict Tenga, Ndolanga ndani TFF

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Marais wa zamani wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga na Leodgar Tenga ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo unaofanyika ukumbi wa AICC jijini Arusha. Mkutano huo umeanza mnamo saa 3.55 asubuhi ambapo jumla ya agenda 14 zitajadiliwa. AlhajiĀ  Ndolanga na Tenga waliwasili kwenye ukumbi wa Mbayuwayu kunakofanyika mkutano huo mnamo saa 3.30 na walikwenda moja kwa moja kwenye chumba cha wageni maalum kilichokuwa jirani na ukumbi huo. Viongozi hao waliambatana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetileh Osiah.

Chanzo: mwananchi.co.tz