Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo Warriors kujipima kwa Misri

C197b64d88a5e3ea4b7900c4776d0d39.png Tembo Warriors kujipima kwa Misri

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye Ulemavu ‘Tembo Warriors’ itacheza mchezo ya kirafiki na timu ya taifa ya Misri Novemba 12, mwaka huu.

Tembo Warriors ipo kambini kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Canaf) yatayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 26 hadi Desemba 5, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Moses Mabula alisema wamepata mwaliko kutoka Shirikisho la Misri hivyo timu itasafiri na wachezaji 14, makocha wawili na viongozi sita wakiwemo kutoka serikalini.

“Tumepokea vizuri mwaliko huu kwani itatusaidia kujenga mahusiano, kujitangaza zaidi na kuinoa timu yetu kwani haijapata mechi za kimataifa za kujipima nguvu,” alisema Mabula.

Misri ni moja ya timu zitakazoshiriki mashindano ya Afrika yatayofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nchi zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni bingwa mtetezi Angola, Nigeria, Liberia, wenyeji Tanzania, Cameroon na Sierra Leone.

Nyingine ni Kenya, Ghana, Morocco, Ethiopia, Uganda, Misri, Zanzibar, Gambia, Togo na Rwanda.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Mamati ya Maandalizi, Riziki Lulida alisema ameridhishwa na maendeleo ya maandalizi na kamati inaendelea kutafuta fedha kwani mashindano yanahitaji zaidi ya Sh milioni 600 pamoja na safari ya Misri

Katika mashindano hayo timu nne zitakazoshika nafasi za mwanzo zitakuwa zimefuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Uturuki, mwakani

Chanzo: www.habarileo.co.tz