Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Teknolojia yawaumbua ‘wapigaji’ viingilio uwanja wa Mkapa

E1fa30a637c7541a747fcdae64ed2177 Teknolojia yawaumbua ‘wapigaji’ viingilio uwanja wa Mkapa

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Teknolojia mpya ya ukusanyaji wa mapato iliyoanza kutumika Uwanja Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam, imeisaidia Serikali kuongeza mapato yanayotokana na viingilio vya mashabiki katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza leo, mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas amesema uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kufungwa mashine ya kulipia fedha katika uwanja huo kumeondoa wizi wa mapato kwa kiasi kikubwa.

Dk Abbas alitolea mifano wa baadhi ya michezo ambayo mapato yalikuwa kiduchu kabla ya kufungwa kwa mashine hizo kuwa ni mchezo wa msimu uliopita kati ya Yanga dhidi ya Namungo ambapo kiasi cha Shilingi milioni saba tu ndicho kilikusanywa.

Dk Abbasi amefafanua zaidi kuwa baada ya teknolojia hiyo kuanza kutumika, mapato baina ya timu hizo yamengozeka msimu huu na kufikia Shilingi milioni 37, baada ya kufungwa mashine hizo.

Katibu Mkuu ameeleza zaidi kuwa mchezo mwingine kati ya Yanga na Tanzania Prisons uliochezwa mwaka jana uliingiza kiasi cha Sh milioni 18 na baada ya kuwepo kwa mfumo huo mapato yameongezeka hadi kufikia Shilingi milioni 81, msimu huu.

Chanzo: habarileo.co.tz