Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameonekana kuwa na mapenzi makubwa ya kumiliki magari ya kifahari.
Miongoni mwa magari hayo ya kifahari ambayo anamiliki mchezaji huyo ni pamoja na Porsche Panamera Turbo Techart ambalo thamani yake ni paundi 140,000 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya milioni 442.
Porsche Panamera Turbo Techart
Lamborghini Aventador ambalo thamani yake ni paundi 270,000 sawa na zaidi ya milioni 853 kwa fedha za kitanzania na Ferrari 812 Superfast ambayo ina gharimu paundi 250,000 (zaid ya milioni 790).
Lamborghini Aventador
Ndinga nyingine ya kifahari ambayo anamiliki Aubameyang ni Range Rover Sport Mansory ambayo thamani yake ni paundi 150,000, ni zaidi ya shilingi milioni 474 kwa fedha za kitanzania.
Ferrari 812 Superfast
Range Rover Sport Mansory
Magari mengine ambayo anamiliki Aubameyang ni:
Audi R8 V10 Plus – £128,000
Aston Martin DB9 Volante 2 – £140,000
Ferrari 488 Spider – £205,000
Porsche Panamera Mansory C One – £113,000
Volkswagen Beetle Cabriolet – £22,000
Porsche Cayenne Techart Magnum – £60,000
Ferrari 458 Italia – £200,000
Audi R8 2013 – £128,000
Lamborghini Gallardo LP560-4 – £141,000