Mara baada ya zoezi hilo la vipimo kukamilika wawili hao Anthony Joshua na Joseph Parker kila mmoja amepata kuzungumza na vyombo vya habari na ndipo tambo zikaanza.
Wakati mabondia hao walipokutana hii leo kwenye zoezi la kupima uzito Cardiff
Picha: Anthony Joshua na Joseph Parker wakutana uso kwa uso kabla ya pambano lao Jumamosi hii
Najiskia vema, mazoezi yangu yamekwenda vizuri nadhani umeona mwenyewe nimepungua hadi kilo. Kupungua kwangu uzito kutaniongezea kuwa mwepesi na haraka zaidi kuliko hata mwanzo.Kwa upande wa Joseph Parker amesema kuwa yupo tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kupigwa hapo kesho siku ya Jumamosi.
Mpinzani wangu namuona yupo vizuri na nibingwa wa dunia ila nitafanya vizuri usiku wa kesho mwenye utashuhudia na nimejiskia furaha kuonana nae uso kwa uso kama hivi. Mimi ni bingwa wa dunia kwa hiyoa akilini mwangu najua naenda kukutana na bingwa mwenzangu wa WBO.
Kabla ya pambano dhidi ya Anthony Joshua bondia Joseph Parker amtafuna samaki mbichi
Mpaka hapa tulipofikia kilakitu kimekamilika wachanifikirie kuhusu pambano hili kwa kuwa najua atakuwa yupo makini.Tunafanana, sote tutakuwa na malengo sawa ulingoni hapo kesho nimemuona ni mtu mwenye kujiamini ninaamini ni mpambanaji mzuri.
Parker ameongeza Raundi za mwanzo chochote kinaweza kutokea itategemea kila mmoja ameingia na mpango upi mzuri zaidi ya mwenzake, nipo tayari kwa chochote. Nipo hapa kwa vita utalazimika kufanya kilakitu ili uweze kunipiga.