Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tattoo za Wawa mtaji tosha wa duka uswazi

80887 Pic+wawa Tattoo za Wawa mtaji tosha wa duka uswazi

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

HIVI unajua kuwa tattoo za beki wa kati wa Simba, Muivory Coast Pascal Wawa jumla ya gharama zote zinaweza kuwa mtaji safi wa duka. Hivi karibuni, Wawa aliliambia MCL Digital mwili wake una zaidi ya tatoo 20 na sasa ameweka wazi kila moja gharama yake ni zaidi ya Sh 150,000. Kwa maana hiyo idadi ya tattoo 20, ukizidisha na Sh 150,000 ni sawa na Sh. 3milioni. Hata hivyo, hiyo ni idadi ndogo tu ya tatoo zake kwa sababu zinazidi 20. Katika maisha ya bongo kiasi cha Sh. 3milioni ni kikubwa na inaweza ikabadilisha maisha ya mtu bila shida. Mtaji wa duka lolote kubwa kama la vyakula, nguo, vipodozi na mahitaji mengine, unaweza kufungua bila matatizo yoyote. "Kila moja ni kama Sh 150,000 au inazidi kama nitakuwa nakumbuka vizuri, nafanya hivyo kwa sababu napenda kuchora tattoo,"alisema Wawa. Katika tattoo ambazo Wawa amechora baadhi ni za majina na sura za familia yake. Mfano ana tattoo moja amechora picha ya mtoto wake wa mwisho Noah na nyingine ameandika majina ya watoto wake wote watano.

Chanzo: mwananchi.co.tz