Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tariq ajipigia mahesabu makali Yanga

89197 Tariq+pic Tariq ajipigia mahesabu makali Yanga

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

STRAIKA mpya wa Yanga, Tariq Seif Kiakala amesema ameanza kupata picha ya nini anatakiwa kukifanya ndani ya timu hiyo baada ya kuanza kuhudhuria mazoezini. Yanga imemsajili mchezaji huyo akitokea Dekernes ya Misiri inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ambako alicheza mechi saba za kirafiki na alifunga mabao matano. Amesema Yanga ni klabu kubwa inayohitaji umakini, kujituma na kutambua, jambo alilosema atalifanyia kazi kuhakikisha hawaangushi viongozi waliomsajili. "Jana nilikuwepo mazoezini nimejifunza mambo mengi sana, nilitaka kujua naenda kuanza maisha na watu wa aina gani hivyo nina kitu ambacho kimeniingia kichwani," "Ni timu yenye mashabiki ambao muda wote wanahitaji ushindi, nafasi yangu ndio inatakiwa umakini zaidi kwani ndio itakayowafanya wacheke ama wanunu,"amesema. Kuhusu ushindani wa namba hilo halimuumizi kichwa kwani anaamini viongozi wa Yanga, wameona upungufu ndio maana wameamua kumsajili. "Ukiona viongozi wanamsajili mchezaji basi utambue kwamba anakuwa na umuhimu wake, nimekuja kupambana hayo mengine yataongea uwanjani,"amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz