Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatia huruma kwenye viwango vya soka duniani

490 Stars TZW

Thu, 21 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Tanzania imezidi kudidimia kwenye viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.

 Kupitia taarifa iliyotolewa leo na FIFA, inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka  142 mwezi Oktoba, ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu. Kwa Uganda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA.

Kwa upande wa 10 bora, Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Tanzania ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin .

Chanzo: bongo5.com