Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yashinda medali 9 za dhahabu Afrika

Dhahabu Pic Data Mashindano ya kuogelea yanaendelea Uganda

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Waogeleaji tisa wa Tanzania, wameanza kwa kishindo mashindano ya Afrika ya kanda ya tatu (Cana Zone 3) yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Kampala nchini Uganda.

Waogeleaji hao wametwaa medali tisa za dhahabu ikiwa ni siku ya kwanza ya mashindano hayo.

Romeo Mwaipasi alifungua pazia la medali kwenye mtindo huru (freestyle) mita 800 akiogelea kwa 10.05.65 kwa watoto chini ya miaka 14 na medali hiyo kwenye mita 100 backstroke

Wengine waliotwaa dhahabu ni Collins Saliboko kwenye freestyle mita 800 kwa waogeleaji wa zaidi ya miaka 15.

Muogeleaji huyo pia ametwaa dhahabu kwenye mita 100 backstroke, Natalia Ladha alitwaa medali kama hiyo upande wa wasichana wakati Austin Okore akitwaa medali hiyo kwenye mita 50 na 100 kwenye backstroke.

Filbertha aliibuka kinara kwenye mita 100 backstroke, medali sawa na aliyopata Ria Save kwa washindani wa umri tofauti.

Ria alitwaa medali nyingine ya fedha kwa wasichana kwenye freestyle mita 800 akitumia 11.04.84. na Natalia akitwaa kwenye mita 800 freestyle wakati Lina Goyayi akitwaa medali kama hiyo kwenye mita 100 backstroke.

Delbert Parth Ipilinga na Jayesh Motichand walitwaa medali za shaba kwenye freestyle mita 800.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania, Inviolatha Itatiro amesema wana nafasi ya kushinda medali zaidi kutokana na kikosi walichonancho kwenye mashindano hayo, maandalizi waliyoyafanya na morali waliyonayo.

"Tuna kikosi kipana na wachezaji wetu watashiriki kwenye mitindo tofauti, hivyo tunatarajia kupata medali zaidi kwa waogeleaji wetu leo jioni na kesho," amesema.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa sita ya kanda ya 3 ni moja ya maandalizi kwa timu ya Tanzania kuelekea kwenye mashindano ya dunia yatakayoanza Desemba 16 hadi 22 huko Abu Dhabi, mji mkuu wa Falme za Kiarabu.

Ria na Collins ni miongoni mwa waogeleaji wanne wa Tanzania ambao watachuana kwenye mashindano ya dunia, wengine ni Hilal Hilal na Eunike Fugo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz