Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yakosa medali za Madola 2018

32679 Pic+madola Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwaka 2018 unaelekea ukingoni na matukio mbalimbali ya michezo ya kufurahisha na kuhuzunisha yalitokea.

Gazeti hili linakuletea matukio mbalimbali yaliyojiri ndani ya mwezi Februari mwaka huu.

Februari Mosi

Simba, Yanga zapewa masharti Uwanja wa Taifa

Klabu za Simba na Yanga zilipewa masharti ya kutumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilitoa waraka wa kuzitaka Simba na Yanga kucheza mechi tatu kila mmoja katika uwanja huo na mechi nyingi zote wacheze kwenye Uwanja wa Uhuru.

Februari 2

Nigeria,Morocco zatinga fainali Chan

Nigeria na Morocco zilitinga Fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (Chan).

Nigeria iliifunga Sudan bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali wakati Morocco iliichapa Libya mabao 3-1.

Februari 4

Serikali yatangaza viwanja Afcon

Serikali ilitaja viwanja sita vitakavyotumika katika Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini mwakani.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo alivitaja viwanja hivyo kuwa ni Taifa, Uhuru na Azam Complex vitakavyotumika kwa mechi wakati viwanja vya Bandari, Jakaya Kikwete Youth Park na Gymkhana vitatumika kwa mazoezi.

Februari 5

Timu sita zapanda Ligi Kuu Bara

Biashara United ya Mara, Alliance FC, Mwanza, KMC, JKT Tanzania na African Lyon za Dar es Salaam, ziliungana na Coastal Union ya Tanga, kupanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Katika ligi hiyo Daraja la Kwanza wakongwe kama Athuman Iddi ‘Chuji’, Hussein Sharrif ‘Casillas’, Salvatory Ntebe waliibeba Coastal Union wakati Stephano Mwasika, Adam Kingwande, Abdulhalim Humoud waliibeba KMC.

Februari 7

Basata yalipuliwa Bungeni.

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilisema Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) liliundwa kwa ajili ya kuboresha na kusimamia kazi za wasanii lakini limegeuka kuwa mahakama ya kuwahukumu wasanii. Februari 10

Tenga aula BMT

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, DK Harrison Mwakyembe alimteua Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Tenga kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Tenga lichukua nafasi ya Dioniz Malinzi aliyemaliza muda wake.

Februari 11

Simba yatikisa Caf

Baada ya kuwa nje kwa miaka mitano Simba ilirejea kwa nguvu katika mashindnao ya Afrika kwa kuishinda Gendermarie ya Somalia mabao 4-0.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco mawili, Said Ndemla na Emmanuel Okwi.

Februari 14

Wanariadha tisa wang’olewa Madola

Wanariadha tisa wakiwemo Emmanuel Giniki na Magdalena Shauri waliondolewa katika kambi ya timu ya Taifa ya Riadha iliyowekwa jijini Arusha ikijiandaa na michezo ya Jumuiya ya Madola.

Wanariadha hao pamoja na Alphonce Simbu, Joseph Panga, Faraja Damas, Fabiani Joseph, Sesilia Ginoka, Mayselina Mbua na Angelina Tsere.

Februari 14

Nyosso afungiwa

Mzimu wa kufungiwa uliendelea kumuandama beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso baada ya kufungiwa mechi tano na faini ya Sh 1 milioni na TFF kwa kosa la kumpiga shabiki wa Simba.

Februari 14

Ronaldo aweka rekodi

Mshambuliaji wa zamani wa Real , Cristiano Ronaldo aliweka rekodi mpya ya mabao katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga mabao 101.

Februari 22

Rais wa Fifa awasili Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infatino aliwasili Tanzania na ujumbe wake kwa ajili ya mkutano wa Shirikisho hilo huku akiweka wazi jinsi Fifa ilivyofanikiwa kuweka uwazi wa matumizi ya fedha.

Pia Infantino alieleza kuwa siku za nyuma Afrika ilikuwa inapata Dola 26 milioni kutoka Fifa, wakati sasa hivi inapata Dola 100 milioni ili kuinua soka katika bara hilo.

Februari 26

Mashaga ang’olewa BFT

Katibu wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) Makore Mashaga aling’olewa katika wadhifa huo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohammed Kiganja. Mwingine aliyeng’olewa ni aliyekuwa makamu wa Rais Lukelo Wililo na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Februari 28

Lwandamina anukia Zesco

Kocha George Lwandamina alihusishwa kutimkia Zesco United ya Zambia baada ya kudaiwa kutokuwa na furaha ndani ya klabu ya Yanga.

Magazeti ya Zambia yaliandika kuwa kocha huyo alikuwa mbioni kutua ndani ya klabu hiyo ambayo aliwahi kuinoa zamani kabla ya kujiunga na Yanga. Hata hivyo baadaye aliondoka kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu Zambia.



Chanzo: mwananchi.co.tz