Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yafuzu Afcon ufukweni

E72b2aac8f6cdb457d78aba5dabf1de3 Tanzania yafuzu Afcon ufukweni

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya soka la Ufukweni imefuzu kucheza fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika Senegal licha ya kufungwa na mabao 6-4 na Burundi katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye fukwe za Coco Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo ambao Tanzania walikuwa wenyeji imefuzu kwa jumla ya mabao 12-9 baada ya ushindi wa mabao 8-3 waliopata katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika fukwe hizo hizo baada ya Burundi kuomba kucheza mechi zake Tanzania kwani uwanja wao umejaa maji.

Katika kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya 2-2, kipindi cha tatu Burundi walikuwa mbele kwa mabao 3-2 na kipindi cha mwisho walimaliza wakiwa mbele kwa 6-4.

Hii ni mara ya pili Tanzania kufuzu baada ya kufanya hivyo mwaka 2018 katika fainali zilizofanyika Sharm el Sheikh nchini Misri.

Wachezaji wanaunda kikosi kilichofuzu ni Ahmed Juma, Fikirini, Abdalah Ramadhan, Erick Manyama, Rolland Msonjo, Kashiru Salum, Jaruph Rajab, Yahya Tumbo, Abdulkadir Talib, Ahmada Abdi,

Wengine ni Mashoto Said, Hakim Mohamed, Kassim Haji, Benai Mapunda, Ibarahim Ibada, Danny Mwanyukule, Juma Kombo, Hamis Said, Samwel Mauro, Stefano Nkomola

Chanzo: www.habarileo.co.tz