Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ya 16 msimamo wa medali Madola

Timu Madola Timu ya wanariadha wa Tanzania iliyopo kwenye mashindano ya Mbio za Jumuia ya Madola

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Tanzania ni miongoni mwa nchi 22 ambazo zimeshinda medali hadi jana Julai 31, ikikamata nafasi ya 16 kwenye msimamo katika michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Uingereza.

Hadi saa 8 mchana, Australia ilikuwa kinara wa medali ikiwa na dhahabu 13, fedha 9 na shaba 12 ikifuatiwa na wenyeji Uingereza yenye dhahabu nane, fedha 13 na shaba nne.

New Zealand ni ya tatu kwenye msimamo ikiwa na dhahabu saba, fedha nne na shaba mbili.

Katika nchi za Afrika, Afrika Kusini ndiyo inaongoza kwa medali hadi sasa ikiwa na dhahabu mbili, haina fedha wala shaba huku kwenye msimamo wa Madola ni ya nane.

Uganda ni ya 10 ikiwa dhahabu moja, wakati Kenya ikiwa ya 14 kwenye msimamo huo na medali ya shaba na fedha.

Kwenye msimamo huo, Tanzania ni ya 16 sawa na Maurtius, Papua New Guinea, Samoa na Singapore ambazo zote zina fedha moja.

Juzi Alphonce Simba aliing'arisha Tanzania baada ya kushinda medali hiyo kwenye mbio ya marathoni mjini Birmingham kwenye michezo hiyo iliyoingia siku ya nne leo.

Wanamichezo wengine Watanzania wataendelea kuchuana leo katika mbio za uwanjani, sanjari na mabondia Kassim Mbundwike na Yusuf Changalawe, wanajudo, mnyanyua vitu vizito, Yohana Mwila na waogeleaji, Collins Saliboko na Kayla Temba.

Chanzo: Mwanaspoti