Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji wa Karate Afrika Mashariki

8e070466641f040b5373abf00e234ceb.png Tanzania mwenyeji wa Karate Afrika Mashariki

Sun, 4 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa Karate ya Afrika Mashariki yanayotarajia kufanyika Desemba 12-13 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha mchezo wa Karate, Sensei-Jerome Mhagama alisema mashindano hayo yahusisha timu za Taifa za Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya na nchi nyingine za ukanda huu zitashiriki mashindano hayo yenye lengo la kudumisha ujirani mwema.

“Ni mashi ndano makubwa na maandalizi yanakwenda vizuri. Tunashukuru klabu za hapa nyumbani zinashirikiana na chama kuandaa mashindano haya,” alisema Mhagama.

Pia alipongeza klabu ya Serengeti kwa kuandaa mashindano hayo na kuvitaka klabu nyingine za mchezo huo hapa nchini, kuiga mfano huo.

Alisema Tanzania imekuwa mwenyeji wa mashindano hayo baada ya kuonekana hakuna tena ugonjwa wa corona.

Katika mashindano yaliyofanyika mwaka jana nchini Uganda, wachezaji wa Tanzania Mikidadi Kilindo na Elisiana Katani waliibuka washindi wa mashindano ya kata kwa upande wa wanaume na wanawake.

Chanzo: habarileo.co.tz