Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji mbio za magari za Afrika

13961 Magari+pic TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Madereva nyota kutoka nchi za Oman, Zambia, Kenya na Uganda wamethibitisha kushiriki mashindano ya mbio za magari ya Afrika yajulikanayo kwa jina la Oryx Energies Rally of Tanzania, yatakayoanza Agosti 31 mpaka Septemba 2 jijini.

Mkurugenzi wa mashindano hayo, Satinder Birdi alisema kuwa mbali ya madereva kutoka nje, pia madereva nyota wa Tanzania wakiongozwa bingwa wa kihistoria, Gerald Miller na Dharam Pandya nao watashiriki.

Birdi alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika eneo la Ubena Estate mkoa wa Pwani, madereva kutoka nje ya nchi watawasili siku nne kabla ya mashindano ili kuwahi zoezi la ukaguzi wa magari yao na masuala mengine ya usalama.

Alisema kuwa wanatarajia kuona mashindano magumu yenye ushindani mkubwa kutoka kwa madereva mahiri wa nje ya nchi wanaowania kulitwaa taji la Afrika.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Energies, Sophonie Babo alisema kuwa wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuendeleza mchezo huo nchini kwa kushirikiana na Chama cha Magari Tanzania (AAT) kuhakikisha mashindano ya Afrika yanafanyika nchini kwa ubora wa hali ya juu.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa AAT, Yusuf Ghor aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi huki akiwaomba wakazi wa eneo la Ubena na kote ambako magari hayo ya mashindano yatapita, kukaa mbali na barabara zitakazotumiwa kwa mbio hizo kwa usalama wao.

“Tunawaomba wakazi wanaozunguka eneo la mashindano kuwa makini siku za mashindano kwani chochote kinaweza kutokea, ili kulinda usalama wao, tunawaomba wasisogelee sana barabara hata kama wanashangilia wake mbali ili kuepuka ajali, zisizo za ulazima, maana haya ni mashindano wakati mwingine madereva wananogewa hivyo ni vyema kuchuakua tahadhari, ni muhimu,” alisema .

Chanzo: mwananchi.co.tz