Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania macho kodo kwa Failuna

77464 Tanzaniapic

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

LEO ndio leo katika Jiji la Doha, Qatar wakati mashindano ya mbio za Dunia zitakapofunguliwa Uwanja wa kimataifa wa Khalifa ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 40,000 kwa wakati mmoja.

Katika mashindano hayo ambayo Tanzania inawakirishwa na wanariadha wanne wote wa mbio ndefu ambao ni mshindi namba tatu wa mbio zilizopita, Alphonce Simbu, Stephano Huche, Agustino Sulle kwa wanaume na Failuna Matanga kwa wanawake.

Failuna anaanza kutupa karata yake ya kwanza leo Ijumaa huku Simbu na wenzake ambao bado wapo nchini hadi Oktoba 5, watakimbia Oktoba 6 ambayo ni siku ya mwisho wa mashindano hayo.

Mfukuza upepo huyo ana kazi ya ziada mbele ya Ruth Chepngetich wa Kenya ambaye mwaka jana kwenye mashindano ya dunia ya nusu marathoni kule Hispania alinyakua medali ya fedha, lakini ndiye bingwa wa Standard Chartered Dubai Marathon mwaka huu akitumia muda wa saa 2:17:08 na katika mashindano manne ambayo ameshiriki mwaka huu ameshika nafasi ya kwanza.

Failuna mwenye miaka 26 anatamba na muda wake bora wa saa 2:27:55 lakini ameahidi kupambana na kuipeperusha bendera ya nchi vizuri.

Kabla ya mashindano hayo kufunguliwa kutakuwa na uchaguzi mkuu wa Rais wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF), ambapo Rais wa sasa, Sebastian Coe anamaliza muda wake japo anaruhusiwa kuwania tena kiti hicho, baada ya mkutano mkuu ulioanza jana Alhamisi na Katibu wa RT, Wilhelm Gidabuday akiwa miongoni mwa waliohudhuria.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz