Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania Prisons hatutaki kurudia ya msimu uliopita

71512 Prisons+picha

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nahodha wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile amesema nafasi mbaya ya ligi waliyomaliza msimu uliopita imewaathiri hawataki hali hiyo ijurudie tena msimu huu wa 2019/20.

Nahodha Mpalile alisema timu yao haijawa na matokeo mazuri misimu miwili mfululizo kitu ambacho kimewapa changamoto wachezaji na viongozi kukaa chini na kupanga mikakati ya kuwarudisha katika soka la ushindani.

Alisema wanamshukuru Mungu msimu wao watauanza wakiwa chini ya kocha Mohamed Adolf aliyetoa mapendekezo nyota wa kusajiliwa ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri na kuleta mafanikio ambayo hawakuwa nayo muda mrefu.

"Maandalizi kwa upande wetu yalikuwa mazuri tumeingia kambini mapema na tumepata michezo ya kirafiki ambayo ilikuwa ni muhimu kwetu na kwa mwalimu kufahamu mabadiliko yetu kwa vitendo kwa kucheza michezo ya kirafiki ili aweze kufanyiakazi mapungufu yetu kabla ya ligi kuanza," alisema.

"Timu iko vizuri kikubwa ni wachezaji kuendelea kuwa wamoja na kufanyia kazi kile tunachoelekezwa ili tuweze kufikia mafanikio leo ni kuona timu inamaliza ligi ikiwa katika nafasi tano za kwanza kwenye msimamo kama ilivyokuwa misimu iliyopita," alisema Mpalile.

Chanzo: mwananchi.co.tz