Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania Bara, Zanzibar uso kwa uso Chalenji Uganda

85714 Pic+chalenji Tanzania Bara, Zanzibar uso kwa uso Chalenji Uganda

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Timu za Taifa za Tanzania Bara na Zanzibar zimepangwa kundi moja katika mashindano ya Chalenji mwaka huu yatakayofanyika Uganda kuanzia Desemba 7 hadi 22.

Katika droo ya mashindano hayo iiyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam na kusimamiwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki (Cecafa), Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herous zimeangukia Kundi C pamoja na Kenya na Djibout.

Kupangwa pamoja kwa ndugu hao wawili kunakumbushia mchezo wa hatua ya makundi ya mashindano hayo mwaka 2017 yaliyofanyika Kenya ambapo Tanzania Bara ililala kwa kipigo cha mabao 2-1.

Katika mashindano hayo, Zanzibar ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali ambayo ilifungwa na wenyeji Kenya kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 ndani ya muda wa kawaida wa mchezo.

Katika mashindano hayo mwaka huu, wenyeji Uganda wamepangwa Kundi A pamoja na nchi za Burundi, Ethiopia na Eritrea.

Ni mashindano yatakayoshirikisha jumla ya timu 12 ambapo kutakuwa na nchi mwalikwa ambaye ni nchi ya DR Congo, iliyopangwa kundi B pamoja na timu za Sudan, Sudan Kusini na Somalia.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye alisema wanatarajia mashindano hayo yatakuwa na ushindani wa hali ya juu.

"Tulipokea maombi kutoka nchi za Zambia, Libya na DR Congo zikitamani kushiriki mashindano haya ya mwaka huu lakini tukaamua kuialika DR Congo kwa sababu ni nchi jirani.

Tunaamini Uganda wamejipanga vizuri kuandaa mashindano hayo kama ambavyo wamefanikiwa katika mashindano ya nyuma ambayo walikuwa wenyeji," alisema Musonye.

Makundi

Kundi A: Uganda, Burundi, Ethiopia, Eritrea

Kundi B: DR Congo, Sudan, Sudan Kusini, Somalia

Kundi C: Kenya, Tanzania, Djibouti, Zanzibar

Chanzo: mwananchi.co.tz