Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu za kushangaza za Ligi ya Mabingwa Ulaya

Ronald Scores Takwimu za kushangaza za Ligi ya Mabingwa Ulaya

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi imeendelea kuchezwa ambapo jana kila timu shiriki ilikuwa ikicheza mchezo wa pili ambapo kumekuwa na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika baadhi ya mitanange ya usiku wa kuamkia leo.

Submitted by George David on Alhamisi , 30th Sep , 2021 Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo akishangilia bao alilofunga dhidi ya Villarreal usiku wa jana.

Cristiano Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyecheza michezo mingi zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (178) akimpiku mlinda mlango wa zamani wa Real Madrid na FC Porto Iker Casillas (177).

Rekodi aliiweka rekodi hiyo wakati akifunga na bao lake la 136 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villarreal ambapo Manchester United ilishinda bao 2-1.

Katika kundi hilo F, mechi nyingine ilishuhudiwa Atalanta wakikamata usukani walipoinyuka Young Boys kwa bao 1-0 na sasa wamefikisha alama 4.

Bayern Munich ilishinda mechi ya pili mfululizo hatua ya makundi wakipachika mabao 8 katika michezo hiyo ambapo jana waliitandika Dynamo Kiev kwa bao 5- na ikumbukwe katika mechi ya kwanza walishinda 3-0 dhidi ya Barcelona.

Stori kubwa imeendelea kumzunguka mshambuliaji Roberto Lewandowski ambaye jana alifunga mabao mawili, ambayo yanamfanya awe amefunga katika michezo sita mfululizo ya michuano hiyo,na lilikua bao lake la 116 katika michezo 100 ya mashindano yote hivi karibuni.

Mabao mengine ya Bayern yalifungwa na Leroy Sane,Serge Gnabry na Eric Maxim Cjoupo Moting na kuwafanya The Bavarians kuongoza kundi E wakiwa na alama 6.

Kwa mara ya kwanza katika historia yao Barcelona imepoteza mechi mbili mfululizo za makundi baada ya kunyukwa na Benfica bao 3-0, sawa kabisa na kipigo walichokipokea kutoka kwa Bayern Munich na sasa wapo mkiani mwa msimamo wa kundi E.

Darwin Nunez alifunga mara mbili na Ferreira Silva ndio waliopeleka kipigo hicho ambacho kimezua sintofahamu katika viunga vya Barcelona.

Kunako kundi H, Federico Chiesa alifunga bao lake la pili katika msimu huu ndani ya Juventus wakati kibibi kizee kikiwapa kipigo mabingwa watetezi Chelsea cha bao 1-0.

Juve ambayo haijaanza vyema Serie A, imepata ushindi wa pili na wanaongoza kundi wakiwa na alama 6, wakifuatiwa na vilabu vya Chelsea na Zenit st petersburg wenye alama 3 kila moja huku Malmo ikishinda nafasi ya mwisho wakiwa hawana alama.

 

Chanzo: eatv.tv