Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru imeziomba funguo za ofisi ya Aveva kwa ajili ya upelelezi

184 WhatsApp Image 2017 12 14 At 13.56.39 660x400.jpeg TZW

Thu, 14 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuomba funguo za ofisi, Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ili wapate nyaraka za upelelezi.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika.

Swai alidai kuwa wanaomba ufunguo kutoka kwa mshtakiwa wa kwanza Aveva ili waweze kupata nyaraka ikiwa sehemu ya kukamilisha upelelezi. Alieleza kuwa Aveva alikuwa na ofisi mbili ya Simba na binafsi na kwamba katika ofisi  hiyo binafsi kuna nyaraka za Simba.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi, Evodius Mtawala aliieleza mahakama kuwa  Aveva ameipata barua hiyo na kwamba juhudi zinaendelea kufanyika na nyaraka zilizoombwa zinaendelea kukusanywa na zitawasilishwa hivi karibuni.

Baada ya kutolewa maelezo hayo,Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi ndani ya siku 14 ili pande hizo zote zikamilishe taratibu hizo, kesi imeahirishwa hadi December 28,2017.

MAHAKAMANI: Kesi ya Aveva na Malinzi

Chanzo: millardayo.com