Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yajiweka njiapanda safari ya CHAN2020

76846 Pic+starsss

Mon, 23 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taifa Stars kimejiweka katika mazingira magumu kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) baada ya kukubali kulala kwa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Sudan kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars italazimika kujilaumu yenyewe kwa kushinda katika lango ka Sudan, lakini ubutu wa safu ya ushambuliaji ndio kilichoimaliza timu hiyo.

Dakika ya saba tu Stars wakifanya shambulizi kali kiungo Mzamiru Yassin kupoteza nafasi ya kufunga kwa kichwa kwa mpira wa adhabu wa beki Erasto Nyoni.

Wageni walijibu mapigo wakifanya shambulizi zurj dakika ya 13 shuti la mohamed Mahamoud linatoka nje akipokea pasi ya Yasir Mohamed aliyenufaika na kiungo Jonas Mkude kupoteza mpira katika eneo la la kati.

Stars ilifanya shambulizi kali dakika ya 15, Ayoub Lyanga alipowapiga chenga mabeki lakini wanashindwa kufunga mabeki wanaokoa akipokea krosi ya Mzamiru.

Kipindi chote cha kwanza Stars ilionekana kuhamia lango ka Sudan, lakini mashambulizi yake hayakuweza kuwa na madhara ya kupatikana kwa mabao.

Pia Soma

Advertisement
Mpaka mapumziko timu zote hazikuweza kupata bao licha yq Stars kutawala kipindi chote.

Kipindi cha pili Stars wakiendelea kulisakama lango la Sudan dakika ya 52 shuti la mpira wa adhabu ya beki Boniface Maganga lilipanguliwa na kipa likitaka wavuni na mabeki kuokoa kisha mpira kumkuta tena kiungo Jonas Mkude na kuiga shuti kali lakini kipa anadaka.

Sudan wakicheza soka la taratibu na hesabu kali walifanikiwa kupata bao kupitia shambulizi la kushtukiza walifanikiwa kupata bao likifungwa na mshambuliaji Yasir Mohamed akimalizia mpira wa shuti lake la awali lililogonga mwamba na kumkuta tena mwenyewe akipokea krosi safi ya mwenzake Ramadan Sharef.

Kuingia kwa bao hilo mashabiki walianza kupiga kelele wakionyesha kuhitaji kufanyika kwa Mabadiliko katika washambuliaji wa Stars na benchi la ufundi baadaye kidogo kumtoa Lyanga na nafasi yake ikichukuliwa na Miraji Athuman.

Dakika ya 71 kiungo Abubakar Salum Sure boy almanusura aisawazishie Stars shuti lake kali linagonga besela na kurudi uwanjani na mabeki wanaokoa.

Dakika ya 72, Stars walimtoa Mzamiru nafasi yake ikichukuliwa na Hassan Dilunga.

Dakika ya 84 Chilunda ambaye hakuonekana kuwa na makali alipiga shuti kali akiwa eneo zuri lakini kipa alikuwa imara na kudaka.

Mpaka mwisho wa mchezo Stars walilala kwa bao 1-0 mechi ya marudiano itachezwa Oktoba 18, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz