Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa ya Bodi ya Ligi kuhusu timu zitakazoshindwa kujitangaza 2021/2022

91dcbe3829a2cf8d925d368144ed3d31 Taarifa ya Bodi ya Ligi kuhusu timu zitakazoshindwa kujitangaza 2021/2022

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MTENDAJI Mkuu wa bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo, amesema msimu ujao wamepanga kuitangaza zaidi Ligi Kuu kwa kuweka mabango 39, uwanjani na timu itakaidi agizo hili itakumbana na adhabu.

Mabango hayo yatatoa nafasi kwa timu kujitangaza na kuitangaza ligi ni manne kutoka bodi, manne kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), timu itayokuwa nyumbani inapaswa kuwa na mabango yake 10 na mdhamini mkuu anapaswa kuwa na mabango 12.

Mabango mengine yanayopaswa kuwa uwanjani, matano kutoka Azam Media na benki ya KCB ambayo ni miongoni mwa wadhamini wataweka mabango manne.

Akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyoandaliwa na ofisi yake, Kasongo, alisema msimu uliopita timu nyingi hazikutekeleza lakini mwaka huu ni lazima na timu yoyote itakayokiuka utaratibu itakutana na adhabu.

“Matangazo yanaongeza thamani ya timu hivyo timu zote zinapaswa kujitangaza tofauti na msimu uliopita hii ni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara na kama timu itakaidi itakumbana na adhabu.

“Nataka nikumbushe klabu zote sababu kanuni hiyo ilisainiwa hivyo yeyote atakayekaidi atakutana na adhabu kwa mujibu wa sheria,” alisema Kasongo.

Wakati huo huo Kasongo, alisema ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kutoka wiki hii na itakuwa na michezo 240

Chanzo: www.tanzaniaweb.live