Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yazipongeza Copco, Baga Friends, Nyaishozi

37c6172616d25a9761eb2765dd714d50 TFF yazipongeza Copco, Baga Friends, Nyaishozi

Wed, 28 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amezipongeza timu za Copco Veterans, Baga Friends na Nyaishozi kwa kupanda Ligi Daraja la Pili (SDL) kutoka katika mashindano ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Ilulu, Lindi.

Fainali za RCL zilianza Aprili 16-25 zikishirikisha timu saba baada ya timu ya Mtwuvila ya Iringa kushindwa kufika kituoni.

Akizungumza na HabariLEO jana, Karia alizitaka timu hizo kufanya maandalizi mazuri ya kucheza Ligi Daraja la Pili pamoja na kuimarisha vikosi vyao ili ushindani walionesha kwenye RCL wakaoneshe pia kwenye ligi hiyo na kuleta changamoto.

“Mkaweke misingi kwenye soka la vijana na kutengeneza timu ambazo zitashiriki kwenye ligi za vijana zinazoendeshwa na TFF.”

“Kipekee niwapongeze Copco Veterans kwa kuwa mabingwa wa RCL 2021,” alisema Karia.

Fainali za RCL zilishirikisha mabingwa Copco Veterans (Mwanza), Baga Friends (Pwani), Nyaishozi (Kagera), Temeke Squad (Dar es Salaam), TMA Stars (Arusha), Black Stars (Tabora) na Lindi United (Lindi).

Chanzo: www.habarileo.co.tz