Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yaweka msimamo Yanga

30030 Pic+TFF TanzaniaWeb

Tue, 4 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imekubali kushirikiana na Kamati Mpya ya Uchaguzi ya Yanga, lakini ikaonya hakuna kitakachobadilika wala kuongezeka.

Wiki iliyopita uongozi wa Yanga ulitangaza wajumbe wapya wa Kamati ya Uchaguzi kuelekea uchaguzi wa Januari 13, mwakani ambayo itaundwa na Mzee Jabiri Katundu, Daniel Mlelwa, Mustafa Mapande, Samuel Mangesho, Samwel Mapande, Edward Mwakingwe na wakili Godfrey Mapunda.

Akizungumzia uteuzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Ally Mchungahela alisema viongozi wa Yanga waliwashirikisha jambo hilo na baada ya uteuzi huo waliwaandikia barua ya kuwajulisha na wamekubali.

“Tunafahamu kuhusu uteuzi uliofanywa na uongozi wa Yanga ambao ulituandikia barua baada ya kuteua wajumbe wao, nasi kupitia taarifa yao tumekubaliana nao bila tatizo lolote,” alisema Mchungahela.

Hata hivyo, Mchungahela alisema mbali na kukubaliana na uteuzi huo, msimamo utabaki kama ulivyokuwa wagombea ni walewale waliopo kwenye mchakato unaoendelea wa uchaguzi bila kubadilishha chochote.

“Tumesimamia mchakato wa uchaguzi kuendelea kama ulivyo ikiwa ni pamoja na wagombea walewale ndio watakaopigiwa kura kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa,” alisema Mchungahela.



Chanzo: mwananchi.co.tz