Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yaongeza nyota wa kigeni Ligi Kuu

11339 Tff+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka saba hadi 10.

Rais wa TFF Wallace Karia alisema wachezaji hao wanaweza kutumika wote katika mechi moja kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.

“Tutaweka kanuni ngumu kwa timu zinazotaka kumsajili mchezaji wa kigeni ili kupata waliokuwa bora na wanaostahili kuwa katika ligi yetu, tupo katika hatua za mwisho kupitia sheria na tutaziweka wazi siku si nyingi, “ alisema Karia.

Rais huyo alisema sheria mpya haitawagusa wachezaji wa kigeni wanaozitumia klabu zao, lakini watakutana na rungu hilo baada ya kumaliza mikataba.

Katika hatua nyingine Kamati ya Utendaji ya TFF imemuondoa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Clement Sanga, baada ya kukosa sifa.

“Yanga ilileta barua ya kukataa kuwa mwenyekiti wao si Sanga ni Yusuf Manji kwa hiyo hana sifa na tutaanza mchakato wa kutafuta mwenyekiti mpya kuziba nafasi, “ alisema Karia.

Sanga ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na kwa sasa anakaimu nafasi ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu.

Pia Karia alisema wataboresha ratiba ya Kombe la FA na wataanzisha mashindano ya ligi kwa vijana chini ya miaka 17 hadi 20.

Chanzo: mwananchi.co.tz