Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yamtetea Morrison, yaiachia Yanga iamue

TFF.png TFF yamtetea Morrison, yaiachia Yanga iamue

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yamshangaa mwamuzi kumzuia kutoka nje ya uwanja, yasema hakuna sheria...

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Bodi yake ya Ligi (TPLB) kwa winga wa kimataifa wa klabu hiyo, Mghana Bernard Morrison kutokakwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba, chombo hicho kinachobeba dhamana la soka nchini, kimemtetea.

Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo:PICHA NA MTANDAO

Katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita na Simba kushinda mabao 4-1, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alimtoa Morrison dakika ya 79 na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana, lakini winga huyo hakukaa katika benchi na badala yake kuamua kutoka moja kwa moja uwanjani na kuondoka.

Wakati anatoka mwamuzi wa akiba alijaribu kumzuia na kumtaka kwenda kukaa benchi na wenzake, lakini Morrison aligoma na kuondoka, jambo ambalo limezua mjadala mzito kutoka kwa wadau wa soka pamoja na vyombo vya habari, huku baadhi ya wachambuzi wakidai ni kosa kisheria.

Hata hivyo, akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati akitangaza tarehe ya mechi ya fainali ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Gwambina FC ya mkoani Mwanza na Dodoma FC, Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo, alisema alichokifanya Morrison si kosa kisheria bali ni suala tu la utovu wa nidhamu.

Kasongo alisema hakuna sheria inayomzuia mchezaji kutoka nje ya uwanja na kudai alimshangaa mwamuzi wa akiba katika mchezo huo alipokuwa anamzuia kutoka nje.

"Kiujumla hajafanya kitendo cha kiungwana, alipaswa kuheshimu mashabiki pamoja na benchi lake la ufundi, lakini alishindwa pia kuwaheshimu wachezaji wenzake na kuamua kutoka nje moja kwa moja, suala hilo litaamuliwa na Yanga wenyewe," alisema.

Aidha, Kasongo aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu pindi wawapo uwanjani ili kujiepusha kupata lawama ambazo hazina maana kutoka kwa mashabiki wao.

Kuhusu fainali ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Gwambina FC ya mkoani Mwanza na Dodoma FC, Kasongo alitangaza kuwa itapigwa Jumamosi wiki hii katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

"Fainali ya kumpata Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza itachezwa Jumamosi hii, tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa wikiendi hii," alisema Kasongo.

Mtendaji huyo alisema michezo ya timu zote ambazo zilishinda nafasi ya pili na ya tatu itachezwa kesho ambapo mchezo wa kwanza utaikutanisha Transist Camp FC dhidi ya Ihefu mechi ambayo itapigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati timu ya Majimaji FC itaumana na Geita FC kwenye dimba la Majimaji mjini Songea, kabla ya timu hizo kurudiana Julai 22, mwaka huu ili kupata timu mbili ambazo zitapambana na timu zinazowania kubaki Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live