Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yalazimisha Uchaguzi Yanga Januari 13, 2019

25581 Pic+tff TanzaniaWeb

Tue, 6 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya mwenyekiti Yusuf Manji, huku likitangaza tarehe ya Uchaguzi huo kuwa ni Januari 13 mwakani.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF, Wakili Ally Mchungahela alisema kuwa suala la uchaguzi wa Yanga ni la lazima na siyo ombi hivyo ni lazima ufanyike.

"Katiba ya Yanga inafafanua wazi kuwa Yanga ni mwanachama wa TFF na itafuata maagizo na maelekezo ambayo itakuwa inapewa hivyo ni lazima ifanye uchaguzi huo na utasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya shirikisho," alisema Mchungahela.

Nafasi ambazo Mchungahela alisema zitajazwa ni ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na zile za wajumbe waliojizulu.

Chanzo: mwananchi.co.tz