Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yakana Wallace Karia sio mfaidika wa pesa za CAF/Ahmad Ahmad

B01C8E85 B62E 4D0F BF5D A053FFB436DE 660x400.jpeg TFF yakana Wallace Karia sio mfaidika wa pesa za CAF/Ahmad Ahmad

Tue, 24 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetoa ufafanuzi kuhusiana yanayoendelea kuwa Rais wa TFF Wallace Karia ni mfaidika wa pesa za Rais wa CAF Ahmad Ahmad ambazo zimemfanya afungiwa na FIFA kwa miaka mitano na faini ya Tsh milioni 510.1.

TFF imesisitiza kuwa ni kweli ziliwahi kutumwa dola 100,000 (Tsh milioni 231.8) ambazo ziliidhinishwa na kamati ya utendaji ya CAF May 2017 na kutaka dola 80,000 (Tsh milioni 185.5) zitumike TFF kwa ajili ya kuendeleza soka na dola 20,000 (Tsh milioni 46.3) zilizobaki ziende kwa Wallace Karia kwa kusaidia shughuli zake za kiutendaji kwa kuwa hana mshahara.

TFF imeeleza fedha hizo ziliingia katika account ya TFF na Karia hakupokea au kuchukua dola 20,000 (Tsh milioni 46.3) kama iliyotakiwa na kuelekeza fedha zote zitumike TFF kwakuwa taasisi hiyo haikuwa vizuri kifedha ila hakuwahi kupokea pesa kutoka CAF/Ahmad Ahmad kupitia account yake binafsi.

Chanzo: millardayo.com