Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yajipanga kuimaliza Cape Verde

17834 Pic+stars TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeandaa mikakati ya kuhakikisha timu ya taifa 'Taifa Stars' inaibuka na ushindi katika michezo miwili mfululizo ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde mwezi ujao.

Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema baada ya Cape Verde kutangaza tarehe ya mchezo wa kwanza, shirikisho limeanza kujipanga ili Stars ivune pointi zote katika mechi hiyo ya ugenini na ile itakayofuata nyumbani.

"Wenzetu Cape Verde wametupa uthibitisho wa mchezo wa kwanza dhidi yao kwamba utakuwa Oktoba 13 na ukizingatia kutakuwa na muda mfupi kabla ya mechi ya marudiano ambayo itachezwa hapa Oktoba 16, TFF kwa kushirikiana na wadhamni ambao ni kampuni ya Bia ya Serengeti tunaangalia uwezekano wa kupata ndege itakayorahisisha usafiri ili kuifanya timu irejee kwa haraka kujiandaa na mechi ya marudiano.

“Pia, tunaangalia uwezekano wa kusaidia mashabiki ambao watataka kwenda kuishangilia timu katika mechi ya kwanza ugenini ili angalau tuwapunguzie gharama waweze kuipa sapoti timu katika mechi hiyo," alisema Ndimbo.

Katika hatua nyingine TFF imetangaza kaulimbiu katika harakati za Stars kuwania kufuzu Mataifa yaAfrika inayosema 'AFCON Cameroon 2019 zamu yetu'.

Chanzo: mwananchi.co.tz