Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yafunguka mkwanja wa Simba

Karia Data TFF yafunguka mkwanja wa Simba

Wed, 28 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya Simba kukabidhiwa kombe la ubingwa wa FA bila zawadi ya pesa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema itakabidhiwa fedha wakati wowote.

Simba imetwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Yanga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, juzi.

Baada ya ushindi huo, Simba ilikabidhiwa zawadi ya kombe bila pesa taslimu Sh50 milioni ambazo hutolewa kwa bingwa.

Jana, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema suala la zawadi ya mshindi lipo chini ya mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi au katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao.

“Lini bingwa wa FA atakabidhiwa zawadi ya pesa hilo linashughulikiwa na mkurugenzi wa mashindano na katibu wao ndiyo wana ratiba ya jambo hilo,” alisema Karia.

Madadi alipoulizwa alisema mchakato wa kukabidhi zawadi kwa bingwa utafanyika wakati wowote na Simba itakabidhiwa pesa zao.

“Ni mapema sana kuzungumzia hili, lakini tayari wamepata kombe na wakati wowote ule watakabidhiwa zawadi ya pesa taslimu Sh50 milioni ambazo hupewa bingwa wa FA,” alisema.

Hata hivyo, hakueleza sababu za Simba kutokabidhiwa fedha hizo sanjari na wakati ilipokabidhiwa kombe la ubingwa juzi, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa timu hiyo kutwaa ubingwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz