Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yaahidi makubwa AFCON utawala wa JPM

39702 Jpm+pict+michez TFF yaahidi makubwa AFCON utawala wa JPM

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Rais John Pombe Magufuli (JPM) amepigiwa chapuo la kuweka historia ya soka kwenye utawala wake. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amewambia wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF unaoendelea mjini hapa kwamba, Shirikisho hilo linataka kuona historia ya Soka inaandikwa kwenye utawala wa JPM. Akizingumza wakati akisoma hotuba yake, Karia alisema anahitaji mkutano mkuu unaofanyika leo mkoani Arusha uwe mkutano wa historia. "Nahitaji Serikali ya JPM ipate nafasi ya kuishuhudia Taifa Stars inashiriki Afcon kwa mara nyingine baada ya ile ya Nyerere (Baba wa Taifa). Alisema maandalizi ya mashindano hayo yataanza mapema baada ya mkutano mkuu unaofanyika leo kwenye ukumbi wa AICC. Taifa Stars inahitaji kushinda kwenye mchezo wao wa mwisho wa Machi 22 dhidi ya Uganda utakaochezwa jijini Dar es Salaam ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kucheza Afcon, rekodi ambayo Tanzania iliiweka mwaka 1979 ilipofuzu na kucheza Afcon ya 1980 ikiwa ni miaka 16 tangu Uhuru 1961.

Chanzo: mwananchi.co.tz