Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF wamsimamisha Kevin Yondani kwa kumtemea mate mchezaji wa Simba

7437 Kwasipic TZW

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Bodi ya Ligi Tanzania imetangaza kumsimamisha beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na tuhuma za kudaiwa kumtemea matena mchezaji wa Simba, Asante Kwasi.



Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo, Boniface Wambura amesema suala hilo limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.

“Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake,” amesema Wambura.

Yondani alionekana kwenye video akimtemea mate Kwasi wakati wa mchezo wa watani wa jadi Jumapili iliyopita ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Loading...
Chanzo: bongo5.com