Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF kukwepa ratiba EPL Ligi Kuu ikirejea

TFF LOGO TFF kukwepa ratiba EPL Ligi Kuu ikirejea

Tue, 19 May 2020 Chanzo: --

WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akieleza kuwa endapo hali ya maambukizo ya virusi vya corona itaendelea kuwa chini ataruhusu michezo kurejea hata wiki hii, Shirikisho la Soka nchini (TFF), limesema kabla ya Ligi Kuu kuanza itabidi kuimulika kwanza.

Juzi Rais Magufuli alieleza kufurahishwa na takwimu za wagonjwa wa corona nchini kupona na kuahidi kama hali ikiendelea kuwa hivyo, ataruhusu vyuo kufunguliwa pamoja kuruhusu michezo iendelee maana ni moja ya burudani kwa Watanzania.

Hata hivyo Rais wa TFF, Wallace Karia, akizungumza na BBC Redio jana, alisema kama serikali ikitoa baraka ya ligi kurejea watahakikisha wanatoa muda wa kutosha kwa timu kujiandaa na ligi hiyo kurejea katikati ya Juni, lakini itabidi kuichunguza kwanza ratiba ya Ligi Kuu England ambayo nayo inatarajiwa kuanza mwezi ujao ili kukwepa mwingiliano.

"Watanzania wanapenda sana Ligi Kuu England, hivyo kama serikali ikiruhusu ligi kurejea, itabidi kuangalia ratiba ya England ili kuzipishanisha na Ligi Kuu Bara, kutoa nafasi kwa mashabiki kuona mechi zote kwa kuwa watakuwa wanaishuhudia kupitia TV," alisema Karia.

Kuhusu afya za wachezaji, alisema wamejipanga kuchukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kushiririsha kamati zote za afya pamoja na wizara husika kwa kuwa TFF inatanguliza kwanza afya za wachezaji mbele pamoja na mashabiki wake.

"Kwanza wachezaji wote watapimwa na tutatoa muda wa kujiandaa, lakini mashabiki hawataruhusiwa kuingia uwanjani watashuhudia kupitia TV, na watakaoruhusiwa ni viongozi wa timu na waandishi wa habari wachache, na tutashirikiana kwa karibu katika kuchukua tahadhari na kamati zetu zote za afya pamoja na Wizara ya Afya," alisema.

Chanzo: --