Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF, klabu zampongeza na kumkaribisha Gekul

Geku; TFF, klabu zampongeza na kumkaribisha Gekul

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alitangaza Baraza la Mawaziri juzi katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, na kumtaja Gekul ataungana na Waziri Innocent Bashungwa katika wizara hiyo.

Katika salamu za pongezi, TFF imesema inamtakiwa kila la kheri Gekul katika kutekeleza majukumu yake na inaahidi kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo.

"Hongera, tunakutakia kila la kheri katika majukumu yako mapya," ilisema kwa kifupi taarifa ya TFF.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema klabu hiyo inampongeza Gekul na inafahamu ni mmoja wa watendaji wazuri na hawana shaka naye.

"Tunamkaribisha na tayari tumeshaandika barua ya pongezi, kuanzia leo (jana), wakati wowote anaweza kuipata ofisini kwake Dodoma na tunamtakia kila la kheri na majukumu yake mapya, tumefurahi pia kupata tena waziri mwanamke kama ilivyokuwa kwa awamu iliyopita tulivyokuwa na Juliana Shonza," alisema Bumbuli.

Kwa upande wa Azam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Thabit Zacharia, alisema yeye binafsi pamoja na klabu yake wanampongeza Gekul na wanamshukuru Naibu Waziri aliyeondoka, Abdallah Uledi ambaye walifanya naye kazi vizuri japo ni kwa muda mfupi.

"Tunampongeza na tunamkaribisha, tunamwambia tutampa ushirikiano na lengo ni kupata mafanikio katika sekta ya michezo, hususani mpira wa miguu," alisema Zacharia.

Kiongozi huyo alisema mara nyingi mawaziri wanawake kwenye wizara hiyo wamekuwa wapambanaji mno ambapo alikumbushia enzi za Fatma Said Ally ambaye alihudumu katika kipindi cha katikati ya miaka ya 1980 ilipojulikana kama Wizara ya Utamaduni wa Taifa, Vijana na Michezo.

"Mama yule (Fatma), alipambana sana kwa kiasi kikubwa hata kuutatua mgogoro mkubwa wa Yanga Ukuta na Yanga Katiba ulipopamba moto wakati huo, lakini namkumbuka mama mwingine, Dk. Fenella Mukangara ambaye naye alikuja kuwa waziri wa michezo, ndiyo maana nasema wanawake wana historia nzuri kwenye michezo." Alisema Zacharia.

Gekul amechukua nafasi ya Ulega ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Chanzo: ippmedia.com