Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF, TBLB Yaingia Makubaliano Na Azam Tv Miaka 10

Azamsports2 190896954 335584121513354 8753769521150680877 N?fit=639%2C426&ssl=1 TFF, TBLB Yaingia Makubaliano Na Azam Tv Miaka 10

Tue, 25 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10.

Makubaliano hayo ambayo wameingia nao yana thamani ya Shilingi bilioni 225.6.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na viongozi waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ya kutia saini mkataba wa Haki za Television, (Tv Rights) katika Hotel ya Hyat iliyo Posta, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema:”Nachukua fursa hii kuwapongeza Azam Media Limetide chini ya Mkurugenzi wao Tido Muhando kwa kufanikiwa kushinda tena zabuni hii hivyo kufanya kazi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania, chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuendesha ligi hii,”.

Chanzo: globalpublishers.co.tz