Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF: Ligi Kuu Bara kusonga kama kawaida

12107 Pic+tff TanzaniaWeb

Wed, 15 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Ligi itaanza kama ilivyopangwa na watakuja kuwatangaza wadhamini wakati ikiwa inaendelea. 

Wambura alisema wapo katika mazungumzo na makampuni mengi ambayo kati ya hayo mdhamini wa msimu uliopita kampuni ya mtandao ya Vodacom ni miongoni mwao. 

Anasema sababu ambayo imepelekea kutuingia mkataba mpya haraka na vodacom ni kutaka baadhi ya mambo muhimu ambayo yalikuwa katika mkataba wa awali yaboreshwe kwanza. 

"Ukiangalia awali Vodacom walikuwa wanatoa jezi pea mbili nyumbani na ugenini na vifaa vingine kama viatu na vingine lakini msimu huo kulikuwa na timu 16 na vifaa vilikuwa havitoshelezi kwa kila timu ndio maana tunataka kama tukisaini mkataba mpya timu zifaidike zaidi ya hapo. 

"Maamuzi ya kuongeza timu tulishirikiana na klabu zote za Ligi Kuu na tulikubalina lakini hata hii si sababu ya kuchelewa kupata mdhamini bali tunataka ambaye tutasaini nae mkataba aweze kutoa zaidi ya vile ambavyo tulikuwa tukipata katika mkataba wa awali. 

"Baada ya kuona changamoto hiyo na Vodacom ambao tupo nao katika mazungumzo tunaongea pia na makampuni mengine kama wanaweza kutupatia zaidi ya hivyo kwani wao kuna faida kubwa wanaipata kama wakiwa wadhamini wakuu, " alisema. 

"Kwahiyo tunaendelea na mazungumzo ambayo kama tutafikia muafaka na kampuni ambayo itatoa vitu ambavyo vinakazi mahitaji muhimu ya kila timu tutasaini mkataba mpya na kumtangaza kama mdhamini mkuu lakini sasa tutabaki na wadhamini wenza waliokuwepo, " alisema Wambura.

Chanzo: mwananchi.co.tz